Jump to content

User:Bitarohize Erick

From Wikipedia, the free encyclopedia

UMUHIMU NA UTARATIBU WA KUWA NA SHERIA NDOGO KATIKA NGAZI YA KIJIJI/MTAA NCHINI TANZANIA

Viongozi wa kuchaguliwa ni nguzo muhimu sana katika maendeleo ya kijiji/kitongoji kwani viongozi hawa wamekasimiwa madaraka ya kusimamia shughuli zote za kimaendeleo kwenye maeneo yao. Utawala wa viongozi wa Serikali za mitaa ndani ya vijiji ni lazima kufuata taratibu na miongozo mbalimbali iliyowekwa ili kulinda dhana ya utawala bora na utawala wa kisheria.

Katika ngazi ya kijiji/Mtaa, ni lazima kuwepo kwa Sheria Ndogo ambazo hutumika kuratibu shughuli zote za kimaendeleo ndani ya kijiji husika. Hivyo kama viongozi wapya wa serikali za mitaa ni muhimu kuhamasisha utungati wa Sheria Ndogo ndani ya vijiji vyenu.

I.          Malengo ya kuwa na Sheria Ndogo

Ni kweli kwamba, Sheria Ndogo zinatokana na mchakato shirikishi ambapo halimashauri ya kijiji husika, hupanga kanuni zinazoweza kutekelezeka ndani ya jamii nzima, na baada ya hapo utaratibu mwingine hufuata wa kupitisha Sheria Ndogo hizo.

Yafuatayo ni madhumuni ya kupitisha Sheria Ndogo katika ngazi ya kijiji;

a.  Kupitia Sheria Ndogo hizo, jamii ya kijijini inaweza kuweka kikamilifu kanuni kwa ajili ya masuala mbalimbali yenye maslahi kwa umma, hivyo huweza kupunguza vitendo vya kuvunja Sheria zinazohusiana na haki na wajibu wa wanakijiji wake.

b.  Kimsingi zinatoa nguvu za kisheria kwa watu ambao wameathirika vibaya na tabia Fulani, pia adhabu na njia dhabiti za udhibiti kuwekwa.

c.  Pia, mchakato wa kupitisha Sheria Ndogo unatoa fursa ya kusimamia matumizi ya bidhaa na huduma za umma, ili kuzuia matumizi mabaya, kulinda matumizi yao ya kijiji uwezo wa kifedha au kiutawala kuhusiana na utoaji wa huduma hizo.

d.  Kwa kwa kuwepo na Sheria Ndogo, serikali ya kijiji hupata uwezo mkubwa wa kusimamia masuala ya maendeleo kijijini na mambo mengine yenye maslahi kwa umma

e.  Sababu nyingine ni kukuza mazingira ya Kisheria, kupunguza migogoro mwa wananchi na kuongeza ustawi wa kijiji kwa ujumla.

II.       Uwezo wa Halimashauri za Vijiji Kisheria

Halimashauri ya kijiji imepewa uwezo kisheria wa kutunga Sheria Ndogo ndani ya mipaka ya kazi iliyopewa chini ya kifungu cha 168 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya) Sura ya 287. Huu ni uwanja mpana sana unawapa fursa wakazi wenyewe wa kijiji husika kuyasimamia masuala yote yanayowahusu wao kama kijiji tu na sis Wilaya au nchi nzima. Kilingana na kifungu cha 113, 114 na 147 cha Sheria za Serikali za Mitaa (Mamlaka ya Wilaya) Sura 287, Halimashauri za kijiji kwa ujumla zina wajibu wa kufanya haya yafuatayo:

·       Kutunza na kuwezesha kudumisha hali ya amani, utulivu na utawala bora ndani ya kijiji

·       Kuzidisha Maendeleo ya jamii na uchumi wa kijiji na vilevile ustawi wa wakazi wake

·       Kulinda mali binafsi na mali ya umma

·       Kuthibiti na Kuboresha Kilimo, biashara na viwanda

·       Kuimarisha maisha ya watu katika afya, elimu na jamii, utamduni na burudani

·       Kupunguza umasikini na dhiki na kuwasaidia vijana, wazee na watu wenye ulemavu

·       Kuanzisha na kudumisha vyanzo vya mapato vyenye uhakika na kuongeza uwajibikaji wa umma katika masuala ya fedha

·       Kutambua na kukuza ufahamu wa masuala ya kijinsia

·       Kulinda na kutumia kwa usahihi mazingira kwa ajili ya maendeleo enedelevu

·       Kupanga na kuratibu shughuli za kijiji na kutoa msaada na ushauri kwa wakazi wa kijijini wanaoshughulika na kilimo, kilimo cha chai, kilimo cha mazao mchanganyiko, misitu au shughuli nyinginezo

·       Kuwahimiza wakazi wa kijijini kuendesha na kushiriki katika shughuli za kijamii

·       Kushiriki, kama vile kwa njia ya ubia katika shughuli za kiuchumi na halimashauri za vijiji vingine

III.    Hitimisho

Kwa sababu Halmashauri hujengwa na uongozi wenu nyie viongozi wa Serikali za Mitaa, hivyo basi Mkurugenzi Mtendaji baada ya shughuli hii ya kuwaapisha atawaagiza wataalam wake wa Sheria ili wafike kwenye vijiji vyenu kuwapeni Semina elekezi itakayohusu jinsi ya Utungaji na Upitishaji wa Sheria Ndogo ngazi ya kijiji sambamba na maeneo muhimu yanayohitaji kutungiwa sheria ndogo.

Imetolewa kwa ajili ya kotoa Semina elekezi kwa wenyeviti wapya wa vijiji na vitongoji baada ya kushinda uchaguzi wa serikali za mitaa.